KARIBUNI BANDARINI ZANZIBAR
Bandari ya Zanzibar sehemu ya abiria kama inavyoonekana hapo juu, imefanyiwa ukarabati mkubwa na kuifanya kuwa bandari ya kisasa na Shirika la Bandari Zanzibar , likishirikiana na kampuni ya Azam Fast Ferry ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu Said Salim Bakhressa.
Kwa wale wanaotarajia kutembelea Zanzibar , kuna vyombo mbali mbali ambavyo vinafaya safari zake kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Boti za kampuni ya Azam ambazo ni Kilimanjaro 1, 2, 3 na 4 huondoka Zanzibar saa moja asubuhi, saa nne asubuhi, saa sita mchana na saa kumi jioni. Pia kuna boti ya Mv Royal ambayo pia hufanya safari zake katika baadhi ya siku.
Kwa nyakati za usiku , kuna boti ya Mv. Flying Horse ambayo huondoka saa tatu usiku kila siku. Pia kuna Meli ya Azam Sea link 1 ambayo huondoka Zanzibar kuelekea Dar Es Salaam kila siku ya Jumapili na Alkhamis.Kwa abiria wa matembezi , Azam Sea link 1 ni mjarabu zaidi lakini huchukua muda mwingi baharini
0 comments:
Post a Comment