Slide Title 1

Aenean quis facilisis massa. Cras justo odio, scelerisque nec dignissim quis, cursus a odio. Duis ut dui vel purus aliquet tristique.

Slide Title 2

Morbi quis tellus eu turpis lacinia pharetra non eget lectus. Vestibulum ante ipsum primis in faucibus orci luctus et ultrices posuere cubilia Curae; Donec.

Slide Title 3

In ornare lacus sit amet est aliquet ac tincidunt tellus semper. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas.

Tuesday, 30 December 2014


MELI YA KOTA TEGUH YAWASILI BANDARINI ZANZIBAR JUMANNE 30/12/2014


Meli hii inaendeshwa na kampuni ya Pacific International Lines (PIL) , inatokea bandari ya JEBEL ALI ya Dubai. 


Meli hii ina kontena 272 zinazotokea nchi mbali mbali. Hivyo wateja wote wa meli hii wanakumbushwa kuwasiliana na mawakala wao ili kukamilisha taratibu za utoaji wa mizigo yao. Kuangalia kama mzigo wako uko katika meli hii unaweza kutembelea tovuti yao /www.pilship.com/tracking.    au unaweza kuwasiliana na 

waendeshaji wa blogu hii kwa email zenjibandarini@gmail.com, unaweza pia kutuma 

namba yako ya kontena katika comment box hapo chini






Monday, 29 December 2014









KARIBUNI BANDARINI ZANZIBAR


Bandari ya Zanzibar sehemu ya abiria kama inavyoonekana hapo juu, imefanyiwa ukarabati mkubwa na kuifanya kuwa bandari ya kisasa na Shirika la Bandari Zanzibar , likishirikiana na kampuni ya Azam Fast Ferry ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu  Said Salim Bakhressa. 


Kwa wale wanaotarajia kutembelea Zanzibar , kuna vyombo mbali mbali ambavyo vinafaya safari zake kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Boti za kampuni ya Azam ambazo ni Kilimanjaro 1, 2, 3 na 4 huondoka Zanzibar saa moja asubuhi, saa nne asubuhi, saa sita mchana na saa kumi jioni. Pia kuna boti ya Mv Royal ambayo pia hufanya safari zake katika baadhi ya siku.


Kwa nyakati za usiku , kuna boti ya Mv. Flying Horse ambayo huondoka saa tatu usiku kila siku. Pia kuna Meli ya Azam Sea link 1 ambayo huondoka Zanzibar kuelekea Dar Es Salaam kila siku ya Jumapili na Alkhamis.Kwa abiria wa matembezi , Azam Sea link 1 ni mjarabu zaidi lakini huchukua muda mwingi baharini

MELI YA AUGUSTE SCHULTE YAWASILI BANDARINI ZANZIBAR


Meli hii inaendeshwa na kampuni ya CMA -CGM DELMAS ikishirikiana na kampuni ya Meli ya EMIRATES SHIPPING. Hivyo wateja wote waliopakia mizigo yao wanashauriwa kuwasiliana na mawakala wao wa forodha kwa ajili ya utoaji mizigo.


Wateja wanakumbushwa kuwa gharama za uhifadhi wa mizigo bandarini ( storage and demurage charges ) zimepanda maradufu. Hivyo mizigo inatakiwa kutolewa haraka iwezekanavyo.


Kujua zaidi mzigo wako unakuja na Meli gani kwa wateja wa CMA-CGM DELMAS  unaweza kutembela tovuti yao www.cma-cgm.com/container tracking . Kwa kampuni ya emirates ni www.emiratesline.com/tracking.